Tupangishe Ltd

Tupangishe Ltd ni kampuni ya kidigitali inayojihusisha na utangazaji wa majengo (vyumba, nyumba na fremu) ya kupangisha katika maeneo yote nchini Tanzania kwa njia ya mtandao. Kampuni hii imekuwa mkombozi kwa wananchi hususan wa Tanzania.

Historia ya Kampuni

Tupangishe Ltd inamilikiwa na Mtanzania, Bwn. Rajabu Bilali Makau, ambaye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni tangu mwaka 2022.

Changamoto za Utafutaji wa Majengo

Zoezi la kutafuta majengo ya kupanga limekuwa changamoto kubwa nchini Tanzania. Wananchi, wanafunzi, wafanyabiashara, na familia kwa ujumla hukumbana na matatizo ya kutafuta majengo kwa kutumia muda mwingi na gharama kubwa.

Wanafunzi

Wanafunzi wa vyuo hupata changamoto za kupata vyumba vya kupanga karibu na vyuo wanavyosoma. Hii ni muhimu kwao ili kuepuka gharama za usafiri na kupata muda wa kujisomea.

Wafanyabiashara

Wafanyabiashara hutafuta fremu za biashara katika maeneo yenye mzunguko mzuri wa wateja. Hata hivyo, mara nyingi wanatumia muda mwingi mitaani bila mafanikio.

Familia

Familia nyingi hupata tabu kupata makazi mapya pindi wanapohama kutokana na ongezeko la kodi au sababu nyinginezo.

Wamiliki wa Majengo

Wamiliki wa majengo hukosa wateja kwa sababu hawajafikiwa na habari kwamba sehemu fulani kuna majengo ya kupanga. Hali hii inawafanya kukaa muda mrefu bila wapangaji.

Madalali

Madalali wa majengo hukumbana na changamoto za menejimenti, ikiwa ni pamoja na kufuatilia wapangaji, malipo, na taarifa za majengo mbalimbali.

Suluhisho Letu

Kwa kutambua changamoto hizi, Tupangishe Ltd imeleta suluhisho la kidigitali kupitia App inayowezesha utafutaji wa majengo kwa urahisi na ufanisi. App hii ni bure kwa watumiaji na inawaunganisha moja kwa moja wamiliki wa majengo na wapangaji.

Lengo Letu

Lengo kubwa ni kufanya maisha kuwa rahisi kwa wananchi wa Tanzania, pamoja na wageni na wawekezaji kutoka nje ya nchi. Teknolojia hii inahakikisha kuwa utandawazi unafanikisha maendeleo kwa kila mmoja.

Pakua App Yetu

App yetu inapatikana mtandaoni. Gusa hapa kuipakua na kufurahia huduma bora za Tupangishe Ltd!

© 2025 Tupangishe Ltd